UVCCM NYAMAGANA YATOA VIFAA NA ZAWADI KWA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA SEKOUTOURE

Posted on: February 24th, 2023

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure imepokwa ugeni wa Vijana wa CCM ukiongozwa na Mhe. Ngw'asi Damas Kamani Mbunge wa Viti maalum kutoka CCM.

Katika ziara hiyo Viongozi hao wa UVCCM wamepanda Miti, kuwajulia hali na kuwapa zawadi mbalimbali wakina mama wajawazito na waliojigungua Watoto. 

Nae Mwenyekiti wa UVCCM Nyamagana Mwanza Ndg. Musa Magana amesema kuwa huduza za hospitali ya Sekoutoure zimeimarika na tuendelee kutunza miundombinu iliyopo. 

Kwa upande wa uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure Bi Lilian Munisi (Katibu wa Hospitali) ametoa shukrani kwa viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi kwa matendo ya huruma kwa wagonjwa, pia ameongeza kuwa huduma bora kwa wagonjwa katika hospitali ya Sekoutoure imeboreshwa zaidi Kwani Serikali inatoa vifaa Tiba vya kutosha na miundombinu bora.