Historia
Wasifu wa hospitali
Hospitali ya Sekou toure ni hospitali ya mkoa wa Mwanza ambayo iko chini ya uangalizi wa Bodi ya hospitali pamoja na Kamati ya Uendeshaji wa Hospitali ya Mkoa (RHMT). Hospitali iko katika wilaya ya Nyamagana, katika Jiji la Mwanza, ilianzishwa mwaka 1994 ikiwa kama hospitali ya Mkoa, kabla ya mwaka 1994 ilikuwa chini ya halmashauri ya Manispaa, ikiwa kama kituo cha afya, Sekou toure ni miongoni mwa hospitali zilizopandishwa hadhi Novemba,2010 kama hospitali ya rufaa ya mkoa. Hospitali ina wodi 9 zenye uwezo wa vitanda 315 na jumla ya watumishi 368 wa kada/sifa tofauti. Hospitali ya mkoa ya (Rufaa) Sekou Toure iko katika daraja la II na inatoa huduma kama hospitali ya rufaa daraja la I.