KATIBU TAWALA WA MKOA WA MWANZA BW. ELIKANA BALANDYA AKIFUNGUA KAMBI YA MADAKTARI BINGWA HOSPITALI YA MKOA WA MWANZA SEKOUTOURE
Posted on: December 5th, 2022Bw. Elikana Balandya amefungua kambi ya madaktari bingwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekoutoure inayofanyika katika viwanja vya hospitali hiyo kuanzia tarehe 05 hadi 09 mwezi desemba 2022.
Amewaasa wananchi wote kutoka mkoa wa Mwanza na Mikoa jirani kujitokeza kwa wingi katika kambi hiyo ili kupata vipimo na matibabu ya kibingwa kwa ajili ya kujenga jamii yenye afya bora