MRADI WA SAFER BIRTH BUNDLE OF CARE (SBBC) WAKAGUA HUDUMA ZITOLEWAZO HOSPITALINI

Posted on: December 8th, 2022

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure Dr. Bahati Msaki amekuatana na kufanya na mazungumzo na wageni kutoka Benki kuu ya Dunia wanaosaidia huduma ya afya ya mama na mtotochini ya mradi wa Safer Birth Bundle of Care (SBBC).


Katika mazungumzo hayo wageni hao kutoka Bank kuu wameupongeza uongozi wa Hospitali kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa. Pia kupitia kikao hicho wawakllishi kutoka Banki kuu na wenye mradi wa WA (SBBC) wamewapongeza watumishi kwa kuendelea kutoa huduma nzuri kwa mama na mtoto kwanikufanya hivyo ni kuisaidia jamii kwa huduma bora.