WAZIRI WA AFYA MH.MOHAMED MCHENGERWA AZINDUA KAMPENI YA IJUE NAMBA YAKO
Posted on: May 6th, 2026Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amezindua rasmi kampeni ya "Ijue Namba Yako" katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza (Sekou Toure). Kampeni hii inalenga kuwahimiza wananchi kupima na kufahamu viashiria muhimu vya afya zao, ikiwemo uwiano wa uzito na urefu (BMI), shinikizo la damu (BP), mapigo ya moyo, pamoja na kiwango cha sukari na mafuta mwilini.
Lengo kuu la hatua hii ni kutoa kinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari na shinikizo la juu la damu, ambayo yamekuwa tishio kwa afya za wengi. Kwa wananchi kufahamu namba hizi mapema, itawasaidia kupata matibabu yakiwa katika hatua za awali, jambo ambalo si tu litaongeza nafasi ya kupona bali pia litapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za matibabu kwa ngazi ya familia na taifa.