WANAWAKE SEKOUTOURE WASHIRIKI SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA VIFAA MBALIMBALI KWA WAGONJWA
Posted on: March 16th, 2023Wanawake Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure wameshiriki tendo la huruma kwa kutoa vifaa mbalimbali kwa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza.
Akiongea kwa niaba ya Watumishi Wanawake wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure Bi. Lilian Munisi katibu wa Hospitali amesaema kuwa tendo la kutoa kwa wagonjwa ni jambo jema linalowatia moyo wagonjwa wakiwa wanapata matibabu katika hospitali yetu.
Zawadi hizo zimetolewa ikiwa ni siku ya wanawake dumiani ambapo wanawake wa hospitali ya Sekoutoure wameshiriki kikamilifu maadhimisho haya.