KITENGO CHA KUSAFISHA DAMU (DIALYSIS) CHATIMIZA MWAKA MMOJA WA KUTOA HUDUMA KWA WAGONJWA

Posted on: March 2nd, 2023

Kitengo cha kusafisha Damu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure kikiadhimisha mwaka mmoja toka kianzishwe mnamo 02/03/2022 chini ya Serikali kupitia Wizara ya Afya.

Mganaga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure Dr. Bahati Msaki amesema kuwa ushirikiano tutaendelea kutoa huduma bora kwa ushirikiano ili kusaidia jamii katika magonjwa mbalimbali, pia amewashukuru watumishi Kwa kuendeleza kufanya kazi Kwa bidii.

 

Kwa upande wa Mkuu wa kitengo hicho Dr. Grahame Mtui amesema katika kitengo Cha kusafisha Damu kitaendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa Kwa sababu Serikari kupitia Wizara ya Afya imetoa vifaa Tiba bora na vya kisasa ambavyo vitasaidia kuimarisha huduma kwa wagonjwa mara wafikapo katika kitengo hiki.

Kitengo hicho kimeendea kumsaidia mgonjwa katika kuboresha afya.