KAMBI YA MADAKTARI BINGWA YAFANYIKA KATIKA HOSPITALI YA SEKOUTOURE - MWANZA

Posted on: December 9th, 2022

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure imefanya kambi ya madaktari bingwa iiliyodumu kwa siku tano kuanzia tarehe 05 hadi 09 mwezi desemba 2022 katika viwanja vya hospitali. Huduma na matibabu mbalimbali vimetolewa.

Huduma ambazo zimetolewa ni pamoja na huduma ya madaktari bingwa kama, daktari bingwa wa tiba, daktari bingwa wa upasuaji, daktari bingwa wa watoto, daktari bingwa wa macho, daktari bingwa wa meno, daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama na uzazi, daktari bingwa wa mionzi, daktari bingwa wa damu, daktari bingwa wa mfumo wa chakula, daktari bingwa wa magonjwa ya akili, huduma za kusafisha damu, huduma ya maabara na dawa.

Wagonjwa mbalimbali wamejitokeza na kupata huduma mbalimbali za kibingwa kutoa kwa madaktari bingwa kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza. 

Jumla ya Madaktari bingwa 20 kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure wametoa huduma katika kambi ya Madaktari bingwa kwa wagonjwa mbalimbali waliojitokeza katika kambi hii iliyofanyika ndani ya viunga vya hospitali.