ELIMU YA USALAMA BARABARANI YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HOSPITALI YA SEKOUTOURE
Posted on: March 22nd, 2023Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kupitia kitengo cha Usalama barabarani kimetoa elimu ya usalama barabarani kwa Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure na kukumbusha majukumu ya usalama barabarani.
Mkufunzi wa elimu hiyo Afande Charles Munthal amesema ajili nyingi zinasababishwa na makosa ya kibinadamu, Ukaguzi wa Chombo cha Moto na hali ya Mazingira hivyo basi katika kuepuka makosa hayo ni vyema kufuata sheria za usalama barabarani.
Mafunzo haya ya nenda kwa usalama barabarani yametolewa kwa lengo la kujenga uelewa na ufahamu wa utumiaji wa vyombo vya moto na watembea kwa miguu na kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali mbalimbali.