How can you reach SekouToure rrh
Ukitoka mjini kati, fuata barabara ya Kenyatta/Nyerere hadi mzunguko wa jengo la CCM mkoa, ndipo utafuata barabara ya kuelekea uwanja wa ndege wa Mwanza (Makongoro) hadi jengo jipya la benki kuu. Utaingia kulia barabara ya Balewa hadi makutano ya barabara ya Balewa na Machemba (eneo la Halmashauri ya Jiji la Mwanza). Hapo utafuata barabara ya Machemba, utapita ofisi za jiji la Mwanza na mbele kidogo upande wa kushoto ndipo ilipo Hospitali ya Sekou Toure.